SSA | Media | Hero | VI24 | Melon tasting in Rwanda

Habari - 05-12-2021

Kuonja tikiti tamu nchini Rwanda

Holland Greentech (HGT) ni wasambazaji wa mbegu za Rijk Zwaan nchini Rwanda. Hivi majuzi walifanya hafla ya kuonja tikiti tamu kama sehemu ya juhudi za kuleta mazao mapya kwa wakulima nchini humo. Gilbert Tuyisenge kutoka HGT Rwanda anatueleza zaidi: "Wakulima wa Rwanda wanasonga mbele kutoka kwa kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo chenye mwelekeo wa soko huku wakijifunza teknolojia bora za kilimo kama vile nyumba kitalu."

Mzunguko wa mazao

"Wakulima wanautumia kitalu nyumba nchini Rwanda na kwingineko wanakabiliwa na changamoto kwa kuwa ni mazao machache tu yanafaa kiuchumi kwa kilimo cha ndani. Hii pia hupunguza fursa katika mzunguko wa mazao. HGT iliamua kuanzisha matikiti matamu kama zao ili kuleta utofauti katika soko,” anasema Gilbert. HGT waliandaa shamba darasa ili kuwaonyesha wakulima kile ambacho kingeweza kufikiwa na walifanya siku ya shambani iliyohudhuriwa vyema, lakini pia waligundua ufahamu wa watumiaji ulihitajika ili kuwasaidia wakulima kutafuta soko la zao hilo.

Kuonja tikiti tamu

Baada ya Maonyesho yenye mafanikio, Holland Green Tech Rwanda iliandaa tukio la kuonja tikiti katika Garden of Eden, soko la mkulima la mboga mboga na matunda lililoko Kigali. Watu wa aina mbali mbali kama watumiaji/walaji, wafanyabiashara na hoteli zilishiriki katika hafla hii.

Maoni chanya

Tukio hilo lilizua shauku kubwa kwa wapita njia na watazamaji waliovutiwa na ukubwa na umbo la bidhaa hii isiyojulikana - kila mtu alitaka kunyakua kipande ili kuonja!

Maoni yalikuwa mazuri sana. Kila mtu alisema kuwa utamu wa matikiti haya ni sehemu au njia ya kuuzia, hivyo kuwapa wakulima uhakika kwamba kutakuwa na soko. Papo hapo, wachuuzi kadhaa na biashara za hotel waliuliza wapi pa kununua matunda haya – hii iliwahamasisha sana wakulima!

Shuhuda za watumiaji

“Sikujua kuwa aina hii ya tikitimaji inapatikana Rwanda. Watoto wangu wanapenda tikitimaji hili tamu la machungwa kama vitafunio vyenye afya," alisema Daniela.

"Ningekuja ofisini kwako kununua mbegu leo kama sikuwa na mkutano, lakini ninafuraha kuwa nimepita hapa. Hii inashangaza na ladha yake si ya kawaida," alisema mkulima RIISH.

"Kupata kitu kingine kitamu na safi ambacho tunaongeza kwenye saladi yetu ya matunda ndio huwafanya wageni wetu waje na tikiti hili ndilo suluhisho. Tumelipenda na wageni wetu pia watalipenda,” alisema ofisa wa Ununuzi wa Hoteli ya Lemigo.

Mawasiliano

Je, ungependa kujaribu tikiti za Rijk Zwaan katika nchi yako? Tafadhali tafuta mwakilishi wa eneo lako hapa

https://www.rijkzwaanafrica.com/sw-ke/mawasiliano